Sep 21, 2012

KIJUE ALICHOSEMA MHADHILI WA CHUO KIKUU CHA SAUT KUHUSU MAISHA YA WASANII WA SWAHILIHOOD






    • USIISHI MAISHA YA KWENYE MOVIE...SIYO HALISI...UTAUMIA.....THIS IS WHAT I USE TO TEACH MY STUDENTS ON MEDIAL AND SOCIAL REALITY.......SOMA HII....

      WENGI wanaamini kuwa maisha ya wasanii wa filamu ni ya kitajiri na kwamba hawana shida kabisa za maisha, hata hivyo ukweli haupo hivyo kabisa. Maisha yao yamejaaa changamoto nyingi na linapokuja suala la wasanii kuendeleza mwonekano wao mbele ya umma, huwagharimu mno baadhi ya wasanii kiasi cha wengi wao kuishi maisha ya kufoji.


      Mpekuzi imegundua kuhusu maisha hayo ya kuigiza kwa wasanii wengi ambao ni nyota katika tasnia ya filamu za Swahiliwood. Mara nyingi wasanii hao wamejikuta wakiingia lawama kutoka kwa baadhi ya ndugu zao baada ya kuombwa misaada kwa kuhisiwa wana uwezo. Wanaposhindwa kutoa misaada hiyo ndipo wanapoingia matatani.


      Hivi karibuni mmoja wa wasanii nyota katika tasnia hiyo aliwaambia wanahabari kuwa wasanii wana maisha mabaya kuliko wanavyofikiriwa. "Jamani msituone hivi, tuna hali mbaya sana. Maisha yetu yamefikia pabaya kwa sababu ya maharamia wa filamu zetu, tunavyoonekana katika filamu si maisha tunayoishi mitaani," alisema."Hatuna hizo fedha wanazofikiria watazamaji wetu, narudia tena maisha yetu mabaya sana." Wasanii wengi wamekuwa wakiishi kwa maisha ya kuigiza kwa kujaribu kujionesha kuwa wana miliki magari ya kifahari wakati ukweli haupo hivyo, japo wengi wanakataa kusema ukweli.

      Maisha hayo yanatokana na wasanii kujaribu kujiweka juu kama walivyo wenzao wa nchi nyingine.

      Inasemekana kuwa wasanii wengi katika tasnia ya filamu za Swahiliwood, wanaishi katika nyumba za kupanga hasa maeneo ya Sinza, Tabata, Mwananyamala na Kijitonyama (kwa Dar es Salaam). Hata wale wanaoishi katika nyumba za familia ni rahisi kukubali hilo iwapo tu nyumba hizo zipo katika maeneo yenye hadhi…..

      By Facebook

No comments:

Post a Comment