Baada ya Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani (FDA) kuidhinisha
dawa ya Truvada kuwa tiba ya kuzuia
kuenea kwa Virusi Vya Ukimwi (VVU).
Dawa hiyo ambayo awali ilikuwa katika kundi la zile
zinazotumiwa kwa ajili ya Kupunguza Makali ya VVU (ARV) sasa imepandishwa chati
wakati ambapo tayari ipo sokoni ikiuzwa kama moja ya ARV za kawaida kwa
shilingi Milioni 1.4 kwa dozi.
Kwa mujibu wa maelezo ya FDA mwathirika anayetumia dawa hiyo anaweza kujamiiana na mwenza wake ambaye hana VVU na hatomuambikiza.
Lakini cha kujiuliza hivi kweli kwa hili Ukimwi utaisha au
ndio itakuwa sehemu ya watu kufanya uzinzi adharani? Mana hivi tu hakuna dawa watu
hawaelewi hatari yake kwa kuendelea kuzini.
Vilevile pamoja na hali yetu tulionayo hasa watanzania wa
hali ya chini tunaoishi kwa dola moja kwa siku ambapo inapelekea kula ya mtu
mwenyewe tatizo sasa kununua dawa hii inayouzwa mamilioni ya pesa ataweza
kweli? Cha msingi hapa ni kwamba serikali yetu iangalie swala hili na
kuwasaidia wananchi wake vinginevyo Ukimwi hautoisha ila matajiri na watu wa
mijini kwa kiasi kikubwa ndio watakao faidika kwa hili kuliko waliovijijini.
No comments:
Post a Comment