May 21, 2012

UTUPWAJI MBAYA WA KONDOM WALETA MAJONZI KWA WAKAZI MWANZA


 Utupwaji ovyo wa kondom zilizotumika umekithili jijini mwanza ambapo watu wengi wamekuwa wakilalamika kutokana na kitendo hicho kimekuwa ni hatari kwa afya za wakazi wa maeneo yao hasa watoto wanapozikuta zimetupwa na kuzichukua kwa kuwa wengi wao hawajui madhara yake.


Hayo yamesemwa na mama mmoja aliependa jina lake atambulike kama mama x alipokuwa anaojiwa na Mtangazaji wa kipindi cha Faraja  radio SAUT FM ya jijini humo kinachoongozwa na Hassan Mrope na Julius Mahela kila Juma pili asubuhi na kusema kuwa utupwaji wa kondom kihilela umekuwa mkubwa sana kutokana na watumiaji kutojari afya za watu wengine ila wanachojari wao ni starehe zao tu na kusahau madhara ya kondom hizo wanazozitupa barabarani na katika maeneo ya makazi ya watu.

Ameongeza kuwa yeye ni mmoja wa watu waliokumbwa na tatizo hilo kwani kati ya watoto wake alionao mmoja ameathilika na ugonjwa wa ukimwi baada ya kuokota kondom akiwa na marafiki zake na kupuliza kama puto bila kujua madhara yake ila kilichomfanya agundue hivyo ni siku alipomuona mtoto wake na wenzie wakipuliza kondom hizo na kadili siku zilivyozidi kwenda mtoto alikuwa anasumbuliwa kiafya ndipo alipoamua kwenda nae kituo cha afya kumpima ndipo ikagundulika ameathilika na virusi vya ukimwi.

Pamoja na hayo, alisema kuwa ni vyema kwa watu wote kuwa waangalifu kwa maeneo wanayochezea watoto wao iliwasije yakawakuta kama yaliomkuta yeye. Vile vile aliwaomba watu makini wanapotupia kondom walizotumia mana sikila mtu hasa watoto wanaojua madhara ya kondom hizo.

No comments:

Post a Comment