Haya yamesemwa
leo na Mwana Hip Hop wa Kitanzania ajulikanae kama NASH Mc alipokuwa akiojiwa
katika kipindi cha Planet Bongo cha East Afrika Radio.
Akuishia
hapo lakini ametolea ufafanuzi kwa yale yote alioyaongelea katika Mahojiano
hayo katika akaunt yake ya Facebook kama ifuatavyo.
“Nawashukuru
sana wale wote waliopoteza muda wao na kusikiliza mahojiano yangu pale East Africa
radio kipindi cha planet bongo,nimezungumza mambo mengi sana lakini wengi
wameonekana kuvutiwa na jambo kubwa na la msingi pale nilipoongelea suala la
matabaka ndani yake kukiwa na ushkaji na umkoa,ambalo linafanywa na baadhi ya
watangazaji na ma dj wa radio”.
“Nimezungumza
yale yanayowagusa wengi ambao hawana sehemu ya kusemea, nimetoa ufafanuzi kua
kila mtu afanye kazi aliyoomba sio unaanza kuponda
au kupendelea wasanii flani,hiyo haipo katika misingi ya taaluma ya
habari,wimbo kama mbovu au mzuri waachie mashabiki wataona wenyewe,usitumie
ukabila au ushakaji kwenye kazi ni rahisi kuwagawa wasanii au watu walio katika
sanaa”.
“Mtangazaji
atangaze,Dj acheze muziki na idara ya muziki isikilize kazi ipeleke kwa dj,kazi
ya kujua huyu msanii mkali au sio mkali watajua mashabiki,tumetoka katika kipindi
kile cha watangazaji na maDj kua mameneja,kina solo thang walipiga sana kelele
wakaonekana wanataka promo lakini madhara yaliporudi kwa wafanyaji ikaonekana
kumbe sio jambo zuri na wamiliki wa vituo vya radio wakapiga marufuku suala hilo
ingawa lipo kwa mbaaali sana”.
“Mimi
nimeamua kulivalia njuga hili suala la ushkaji na umkoa katika radio nyingi tu
nchini mpaka tuone mwisho wake,vipaji vingi vinapotea mtaani kwa matabaka
yaliyojengwa na baadhi ya watangazaji na ma dj wachache wasioutakia mema muziki
huu”.
Na
kumalizia Nash Mc alitoa wito kwa Mashabiki wa Muziki wa kizazi kipya kuwa
wasanii wanapohojiwa watu waulize maswali yenye msingi sio unakurupuka tu swali
la kiwaki na watanzania wengi wamekuwa wanakremu tu vichwa ni mwao kua nyimbo
kali wanatoa wale wasanii waliowazoea tu,kumbe sio ila Wasanii hata
waliowachanga au wasiopata Air time ya kutosha radioni ni wakali sana.
NASH MC a.k.a Mouamar
Ghadafi Naandika 2014!
No comments:
Post a Comment