Mtangazaji wa ITV ajulikanae kwa jina la
Ufoo Saro amejeruhiwa vibaya kwa kupigwa
risasi na mchumba wake ambaye pia alimuu na mama mkwe wake kisha naye alijipiga risasi na kujiua Alfajiri
ya leo.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa kipolisi wa Kinondoni kamanda Wambura amethibitisha tukio hilo alipoongea na Radio One nakusema kuwa Ufoo alipigwa risasi na mchumba wake ambae anafanya kazi katika umoja wa mataifa ( UN ) huko Sudani ila bado haijafahamika kitengo alichokuwa akifanyia kazi.
Habari zinasema kuwa mchumba wake huyo alirudi jana nchini
Tanzania na kufikia nyumbani kwa Ufoo. Hivyo kulitokea ugomvi kati ya wawili
hao ambapo walishindwa kuelewana na ndipo walipoamua kwenda kwa mama mzazi wa
Ufoo Saro(mama mkwe)kibamba kupata suluhu.
Walipofika kwa Mama Ufoo na kuanza kikao cha kutafuta suluhu ndipo ilipoonekana kuwa mwanaume ndio tatizo. Kutokana na hali hiyo, mwanaume alimshutumu mama mkwe wake kwamba amekuwa na mazoea ya kumtetea mwanae, kwa hasira akatoa bastola na kumpiga mama mkwe wake kichwani na kumuua papo hapo.
Baada ya kumpiga Mama Ufoo na kumuua ndipo alipomgeukia Ufoo Saro na kumpiga nae risasi mbili, moja ya tumboni na nyingine ya mguuni na kudhani kwamba amemuua kumbe amemjeruhi tu kisha kujipiga mwenyewe risasi ya kidevuni na kufariki dunia papo hapo.

Kwa taarifa zilizopatikana kuwa, Ufoo Saro anaendelea
vizuri akiwa amelazwa ICU akipatiwa
matibabu katika Hospitali ya Muhimbili.
No comments:
Post a Comment