Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akiwakaribisha nchini wajumbe wa Baraza la
Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia
na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) kabla ya kukabidhiwa uenyekiti
wa RECSA kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchini Rwanda ambaye pia ni
Mwenyekiti RECSA kwasasa, Sheikh Mussa Fazil Harerimana (katikati). Dk Nchimbi
anatarajiwa kuiongoza RECSA kwa kipindi cha miaka miwili. Kulia ni Katibu
Mtendaji wa baraza hilo, Theoneste Mutsindashyaka. Mkutano huo unafanyika
katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Mwenyekiti Baraza la Mawaziri wa
Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti
Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) na Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchini Rwanda,
Sheikh Mussa Fazil Harerimana (katikati) akizungumza na wajumbe wa RECSA
(hawapo pichani) katika mkutano wao unaofanyika katika Hoteli ya Serena, jijini
Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi
ambaye leo anatarajiwa kukabidhiwa uenyekiti RECSA ambapo anatarajiwa kuiongoza
kwa kipindi cha miaka miwili. Kulia ni Katibu Mtendaji wa baraza hilo,
Theoneste Mutsindashyaka. Mkutano huo unafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa
Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Wajumbe wa Baraza la Mawaziri wa
Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti
Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) wakiwa katika chumba cha mkutano wakijadili
masuala mbalimbali ya jinsi ya Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa
Silaha Haramu katika nchi wanachama ambazo ni Burundi, Congo, Djibout,
Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda na Tanzania. Mkutano huo
unafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam
ambapo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (meza kuu-kushoto)
anatarajiwa kukabidhiwa uenyekiti wa RECSA kutoka kwa Mwenyekiti anayemaliza
muda wake leo, Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchini Rwanda, Sheikh Mussa Fazil
Harerimana (meza kuu-katikati). Picha na
Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Wajumbe wa Baraza la Mawaziri wa
Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti
Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya
mkutano wa unaofanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam
kufunguliwa. Wapili kushoto waliokaa ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk
Emmanuel Nchimbi ambaye leo anatarajiwa kukabidhiwa uenyekiti wa RECSA kutoka
kwa Mwenyekiti anayemaliza muda wake, Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchini
Rwanda, Sheikh Mussa Fazil Harerimana (wakatikati). Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
vizuri sana, hongera zako waziri waangu
ReplyDelete