Oct 12, 2013

KING MAJUTO NA UBUNGE MWAKA 2015

Mchekeshaji mkongwe nchini Tanzania King Majuto (65) anategemea kugombea ubunge ifikapo mwaka 2015 katika uchaguzi mkuu kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi(CCM).

Majuto amesema kuwa, Mungu akimjalia afya njema kuufikia kipindi icho basi atagombea ubunge katika jimbo lake la Tanga Mjini, lakini ikishindikana atagombea kwenye wilaya ya Mkinga kwani analifahamu vizuri jimbo hilo na matatizo yanayowakabili wakazi wake.


“Kama Mungu akinijalia afya njema nitagombea ubunge kwa tiketi ya CCM katika jimbo langu la Tanga Mjini ikishindikana nitagombea kwenye wilaya ya Mkinga kwa sababu nayajua matatizo yanayowakabili wakazi wa maeneo hayo, pia napenda kuwa karibu sana na jamii, kwani ndivyo nchi inavyotakiwa kuendeshwa”. Amesema Majuto kupitia page yake ya Face book

Majuto akaongeza kuwa, anaweza kuongoza na kuwasaidia wananchi wenzie wa Tanga kutokana na matatizo yao kama vile tatizo la Maji, Umeme na ugawaji wa viwanja kiujanja ujanja unaofanyika tena kwa watu wachache kisha vinakuja kuuzwa kwa wananchi wa hali ya chini kwa bei ghali sana.

Vile vile amesema hawezi kushindwa kuwaongoza wananchi kisa yeye ni Msanii kwani kuna wenzie wamegombea na wanafanya vizuri katika nafasi zao pamoja ni wasanii kama vile Mh.Joseph Mbilinyi(SUGU) na wengineo waliopo mjengoni Mkoani Dodoma.

Pamoja na hayo, amesema kuwa amatembea sehemu nyingi sana hapa nchini kutokana na sanaa yake, akagundua kuwa Tanzania inamaeneo makubwa sana, mapori kwa mapori tena sio hifadhi kusema watu hawaruhusiwi kulima au kuwekeza katika maeneo hayo, bali ni kutokuwepo kwa usimamizi na utendaji uliobora kwa baadhi ya viongozi wetu pamoja na kujitahidi kwa Rais Jakaya Kikwete kuleta Matrekta yagaiwe kwa wananchi lakini matokeo yake utumika tofauti na malengo lengwa.

No comments:

Post a Comment