Apr 8, 2012

Mwana Mama Toni Braxton akanusha uvumi wa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Eddie Murphy




Mwanamuziki kutoka Nchini Marekani Toni Braxton amekanusha uvumi ulioenea maeneneo mengi nchini humo pamoja na nje ya nchi hiyo kuwa anatoka na Muigizaji Eddie Murphy.
Aliongea hayo alopokuwa anaojiwa katika kipindi cha Wendy Williums kinachorushwa na mwanadada Wendy Joan Williums na kusema kuwa maneno au habari hizo sio za kweli bali zinazushwa na watu wasiopenda maendeleo yake.
Lakini alipokuwa anaojiwa katika kipindi hicho alikuwa na mtoto wake anaeitwa Diezel amabaye alijalibu kuulizwa na Host wa kipindi hiko kuwa kama amewaikumuona Eddie kuja kwao ama kuwa karibu na mama yake.
 Mtoto huyo alishindwa kujibu kutokana na kuwa na kigugumizi juu ya swala hilo ndipo ikaonekana kuna kitu kinaendelea kati ya mastaa hao iliopelekea mtoto wa Toni kushindwa kusema ukweli alipoulizwa swali juu ya uhusiano wa mama yake na Eddie.

Barnaba Boy apata Baby Boy usiku wa kihistoria


Msanii Barnaba Boy anaetamba na ngoma yake “Magube gube” amepata mtoto wa kiume usiku wa kifo cha Msanii wa Bongo movie Steven Kanumba kupitia girlfriend wake na kumpa jina la Steven mtoto huyo ni katika kumuenzi gwiji wa Bongo movie nchini marehemu Kanumba.

Mbali na hayo Barnaba ameongeza kuwa anatarajia kuachia ngoma yake mpya itayoitwa ‘Niombe’ ambayo inazungumzia mapenzi  imetengenezwa ndani ya studio za Ngoma records chini ya Tudy Thomas akiwa ameimba mwenyewe na itatoka siku ya juma pili tarehe 15 mwezi huu.

Apr 6, 2012

Hemedi P.H.D amewatolea uvivu wasanii wa movie nchini Tanzania

MSANII wa muziki na filamu za kibongo, Hemed Suleiman P.H.D, amesema majivuno ya wasanii wakubwa wa  Bongo movie ni sababu moja wapo inayochangia kwa kiasi kikubwa kushusha ubora wa filamu Tanzania.

Ameongeza kuwa wasanii wengi baada ya kucheza filamu kadhaa wanaanza kujiona tayari wametoka na hata wakiitwa kucheza filamu fulani ambayo haina nyota wengi wakubwa wanakataa.

Aliongeza kuwa kwa upande wake hawezi kukataa kucheza filamu hata kama ndani hakuna staa yoyote kwani anaamini chipukizi wengi wana uwezo mkubwa kuliko hata hao mastaa wenyewe.

Amewashauri watu wanaokuwa wakiwatumia sana nyota wakubwa kwa lengo la kuuza filamu zao lakini ukweli ni kwamba hata chipukizi wanauwezo mkubwa wa kucheza na kufikisha ujumbe kuliko hata mastaa hivyo wajaribu kuwatumia wasanii wadogo na sio kuwatenga katika tasnia hii.