Sep 20, 2013

KUMBE HUYU NDIO CHANZO CHA UMASIKINI WA WASANII WA FILAM NCHINI

William Mtitu

Inajulikana kuwa Wasanii wetu wanaigiza Filam nyingi sana lakini mwisho wa siku ukijakufuatilia maisha yao kiundani au wakifariki utagundua siri kubwa sana iliojificha hasa pale utakapogundua kuwa Msanii ameondoka hana Nyumba wala Biashara ya maana inayoendana na umaarufu alionao.
Kwa mujibu wa Wiliam Mtitu ambae anamiliki kampuni ya Filamu ijulikanayo kama 5Effects, amesema kwa kiasi kikubwa  Wasambazaji wa kazi zao ndio chanzo kikubwa cha wao kuwa au kufa wakiwa masikini pamoja na kufanya kazi nyingi sana ambazo kwa uhalisia wake lazima zingemfanya mtu awe na maisha mazuri.
Amesema haya pale alipopost kwenye mtandao wa kijamii kuwa “BILA STEPS

Sep 17, 2013

DAYNA KUTOKA MUZIKI HADI UWANAMITINDO

Mwanamuziki wa kizazi kipya Dayna Nyange a.k.a Dayna kuingia katika mitindo kutokana na chanzo hiki EJ FASHION & MEDIA.Dayna amedai yakuwa hivi karibuni ataingia kwenye tasnia ya fashion akiwa kama mwanamitindo au mbunifu wa mavazi.

Hii imetokana baada ya kuonekana mara nyingi akiwa karibu na mwana mitindo maarufu jokate Mwegelo kwa kuwa ndio rolemodel wake katika mitindo.

Pamoja na hayo, inaonekana katika kubadilishana fani au kuonesha vibaji walivyonavyo wadada hawa kutokana kuwa hivi karibuni nae Jokate ameonekana kuingia katika muziki hasa baada ya kutoa ngoma alioshirikiana na Lucci inayoenda kwa jina la Dada & Kaka
 Dayna Nyange
Dayna & Jokate

Dec 5, 2012

HII NDIO AKAUNTI YA PAPA BENEDICT XVI NDANI YA TWITTER

Wakristo wakatoliki wote ulimwenguni sasa wataweza kujifunza mengi juu ya uwepo wa mungu pamoja na kanisa lao kupitia akaunti ambayo imefungulia na Papa Benedict XVI ambayo madhumuni yake ni kuutangaza ukristo na watu wamjue mungu kupitia jumbe na maswali atakayo kuwa anajibu Papa kutoka kwa watu wote.

Akaunti hiyo ameshaifungua rasmi kama unavyoiona hapo katika picha ya chini ndio itakayokuwa inatumika kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter.

Dec 3, 2012

PAPA BENEDICT XVI AFUNGUA AKAUNTI YAKE KATIKA MTANDAO WA TWITTER


Papa Benedict XVI ameamua kufungua akaunti hii kwa ajiri ya kusambaza ujumbe wa kanisa katoliki na kujibu maswali mbali mbali atakayoulizwa juu ya kanisa hilo pamoja na maswala ya mungu.

Pamoja na hayo Papa atatumia lugha mbali mbali kujibu maswali hayo ili kila mtu aweze kuelewa juu ya Mungu na ukristo.

Kwa mujibu wa BBC Swahili Kanisa hilo la katoliki tayari linatumia mitandao kadhaa ya kijamii na hivi karibuni limezindua mtandao mkuu unaounganisha mitandao ya kanisa hilo kote ulimwenguni.

Wakatoliki kote duniani, wataweza kuwasilina na Papa kupitia Twitter wakati akaunti hiyo itakapozinduliwa rasmi hivi karibuni na itawasaidia kumjua mungu vizuri pamoja na kanisa hilo.

Imesemwa kuwa kuhusu akaunti hiyo taarifa itatolewa baadae leo hii katika mkutano na waandishi wa habari.

Dec 2, 2012

MTANGAZAJI WA TBC1 GRACE KINGARAME AFUNGA NDOA NA MWANDISHI WA HABARI MWENZIE


Mtangazaji wa kituo cha televisheni TBC 1 Grace Kingarame amefunga ndoa na  Julius Kihampa Mwandishi wa habari Mwandamizi kutoka gazeti la Jambo leo katika kanisa la Mt.Albano, Anglicana jijini Dar es salaam leo.
Grace & Mumewe Julius wakionesha vyeti vyao vya ndoa baada ya ndoa yao kubarikiwa au kuhalalishwa.