William Mtitu
Inajulikana kuwa
Wasanii wetu wanaigiza Filam nyingi sana lakini mwisho wa siku ukijakufuatilia
maisha yao kiundani au wakifariki utagundua siri kubwa sana iliojificha hasa
pale utakapogundua kuwa Msanii ameondoka hana Nyumba wala Biashara ya maana
inayoendana na umaarufu alionao.
Kwa mujibu wa Wiliam Mtitu ambae
anamiliki kampuni ya Filamu ijulikanayo kama 5Effects, amesema kwa kiasi kikubwa Wasambazaji wa kazi zao ndio chanzo kikubwa
cha wao kuwa au kufa wakiwa masikini pamoja na kufanya kazi nyingi sana ambazo
kwa uhalisia wake lazima zingemfanya mtu awe na maisha mazuri.
Amesema haya pale alipopost kwenye mtandao wa kijamii kuwa “BILA
STEPS INAWEZEKANA” hasa kutokana na maswali
ambayo akutana nayo kutoka kwa mashabiki wa filam nchini “kwanini ameamua
kusambaza filam zake mwenyewe kupitia kampuni yake ya 5effects wakati kuna
makampuni mengi ya usambazaji wa kazi zao na yenye kujulikana mikoa mingi nchini kuliko
kampuni yake?”
Lakini Mtitu amesema kuwa yeye ndie Msanii wa kwanza kufanya kazi na
kampuni ya Steps lakini matokeo yake mpaka leo hajaona faida yake kwasababu hawatoi malipo ya filamu wanazozinunua kwa muda muhafaka na nunua
haki zote za filamu wanazopelekewa kwa ajili ya kuzisambaza kwa hiyo baada tu
ya kusaini mkataba wao unakuwa huwezi kufaidika tena na chochote kutokana na
mauzo au faida nyingine zinazotokana na filamu yako, hivyo kutufanya tuendelee
kuwa mafukara siku hadi siku.
Ameongeza kuwa hata Marehemu Steven Kanumba pamoja ameigiza filamu nyingi
na kujizolea umaarufu ndani na nje ya Nchi lakini hajaacha filamu wala hana
filamu yeyote iliochini yake baada ya kusaini mkataba na Steps. Ndio maana hata
siku kamati ya Mazishi ya Kanumba ilipoitwa Ikulu kwa rais wa Jamuhuri ya
muungano wa Tanzania Ndugu Jakaya Kikwete alipowauliza Kanumba ameacha filamu
ngapi walishindwa kujibu lakini kwa aibu ilibidi waongee ukweli na kutokana na
jibu walilolitoa rais alisikitika sana.
“Mheshimiwa rais kwa kweli Marehemu Kanumba hajaacha hata filamu moja,
zote ni za msambazaji wake na hata mbili ambazo zilikuwa hazijatoka yaani ‘Ndoa
yangu’ na ‘Love & Power’ tayari zilikuwa ni za msambazaji kutokana na aina
ya mkataba tunayoingia na msambazaji.
Pamoja na hayo, Mtitu aliongeza kuwa nawashangaa watu wanaomshutumu mama
mzazi wa Kanumba kuwa amemaliza mali za mwanae na sasa anaishi kwa kufadhiliwa
na Lulu, wangejua kilicho nyuma ya pazia wangemuonea huruma badala ya
kumshutumu. Wakati Steps wanakiri kuwa filamu iliyowahi kuuza sana katika
historia ya kampuni yao ni ‘Ndoa yangu’ ya Kanumba, hawasemi kuwa familia yake
imenufaika vipi zaidi ya kupewa tuzo.
Mtitu akasema mfano mwingine hai ni wa marehemu Said Juma Kilowoko
(Sajuki) ambaye ni miongoni mwa wasanii maarufu na watayarishaji wa filamu.
Lakini Marehemu Sajuki alilazimika kuzunguka na wasanii wenziye mikoani akiwa
anaumwa taabani ili tu aweze kupata fedha za matibabu wakati amefanya kazi
nyingi sana. Vilevile ilibidi mkewe Sajuki, Wastara
atengeneze ‘Mr & Mrs Sajuki’ ili aweze kupata fedha za kujikimu na zakumuuguza
mumewe.
“Kama tungekuwa hatulazimiki kuuza haki zetu zote, familia hiyo ingeweza
japo kupeleka filamu zake kwenye vituo vya runinga barani Afrika ambako ni
chanzo kingine cha mapato kwa msanii ndio maana nimeamua kujitoa Steps kwa
kuogopa familia yangu isije kudhalilika baada ya kifo changu”.Amesema Mtitu
No comments:
Post a Comment