Kauli
mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “USALAMA BARABARANI UNAANZA NA MIMI, WEWE
NA SISI SOTE”.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara
ya Ujenzi, Mhandisi Gerson Lwenge, akitoa hotuba ya kufunga Maadhimisho ya Wiki
ya Nenda kwa Usalama Barabarani leo yaliyokuwa yakiadhimishwa Kitaifa katika
Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza. Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza Usalama Barabarani, Pereira
Ame Silima, kulia ni Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, DCP
Mohamed Mpinga. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza Usalama Barabarani, Pereira Ame Silima
akitoa hotuba fupi ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi,
Mhandisi Gerson Lwenge (watatu kushoto) kutoa hotuba ya kufunga Maadhimisho ya
Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yaliyokuwa yakiadhimishwa Kitaifa katika
Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza. Kulia ni Kamanda wa Polisi Kikosi cha
Usalama Barabarani, DCP Mohamed Mpinga. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi.
Washiriki wa maonesho, wananchi
mbalimbali wakiingia ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba kwa maandamano ya kufunga maadhimisha
Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani leo. Maadhimisho ya Nenda kwa Usalama yamefungwa
na Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Mhandisi Gerson Lwenge. Picha na Felix
Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Maneja Masoko wa Shirika la Bima
la Taifa (NIC), Elisante Maleko akitoa maelezo kwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa
Wizara ya Ujenzi, Mhandisi Gerson Lwenge (wapili kushoto) ya jinsi ya shirika
hilo linavyotoa bima za magari, mali, maisha na afya wakati alipokuwa
analitembelea banda la shirika hilo katika maonesho ya Wiki ya Nenda kwa
Usalama Barabarani kabla ya kuyafunga maonesho hayo yaliyokuwa yanafanyika
katika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza. Kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama wa Barabarani,
Pereira Ame Silima. Kulia ni Afisa Bima wa shirika hilo Hollo Kazi. Picha na
Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkuu wa Kitengo cha Usalama na
Mazingira kutoka Makao Makuu ya Wakala wa Barabarani Tanzania (Tanroads), Zafarani
Madayi akitoa maelezo kwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi,
Mhandisi Gerson Lwenge (wapili kushoto) jinsi Tanroads inavyoweza kutengeneza
barabara bora na zenye alama za usalama kwa lengo la kuondoa ajali mbalimbali
zinazoweza kutoa barabarani kabla ya kuyafunga maonesho hayo yaliyokuwa
yanafanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza. Watatu kushoto ni Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani,
Pereira Ame Silima. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kamanda wa Polisi Kikosi cha
Usalama Barabarani nchini, DCP Mohamed Mpinga, akikionesha kitabu cha taaluma
ya ufundishaji wa madereva kilichozinduliwa na mgeni rasmi Naibu Waziri wa
Wizara ya Ujenzi, Mhandisi Gerson Lwenge, kabla ya kufunga maadhimisho ya Wiki
ya Nenda kwa Usalama yaliyokuwa yanafanyika jijini Mwanza. Kulia (waliokaa) ni
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani,
Pereira Ame Silima. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkurugenzi wa Radio One, Deogratius
Rweyunga (kushoto) akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na
Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani, Pereira Ame Silima, baada ya
kupokea cheti cha kuthamini mchango wa Radio hiyo iliyopo Dar es Salaam kwa
kutangaza habari mbalimbali za usalama barabarani. Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama
Barabarani yamefungwa rasmi na Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Mhandisi
Gerson Lwenge, jijini Mwanza leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment