Sep 24, 2013

CHEKA NA MNYAMWEZI UONGEZE SIKU ZA KUISHI



Siku moja  Jamaa mmoja alikuwa amechoka kufanya kazi sasa akajifikilia abuni njia gani ili Bosi wake amruhusu kwenda nyumbani?

Baada ya kujifikilia sana mwisho akapata jibu la kujitundika juu ya Bulb na Tai yake, mara akatokea bosi wake na mazungumzo yakawa kama yafuatavyo:

BOSI: wewe unafanya nini huko juu?....
JAMAA: Bosi namulika ofisi…..

Sasa baada ya bosi kuona vile akajua huyu jamaa stress za kazi zinamsumbua sio bure, na hajawai kuona mtu anajitundika eti anamulika ofisi kana kwamba ni Taa , Mwisho akaona amwambie…

BOSI: Ok, basi shuka na uende nyumbani mana inaonesha stress za kazi zinakusumbua kisha urudi kesho….
Jamaa akashuka na kukusanya kilichochake na kuanza kuondoka, Mara akainuka na mfanyakazi mwingine nae akaanza kukusanya vitu vyake na kuanza kuondoka, Bosi alishangaa kuona mfanyakazi mwingine anaondoka wakati hajaruhusiwa, ikabidi amuulize…

BOSI: Sasa na wewe unaenda wapi Wakati nimemluhusu mwenzio?....
JAMAA WA PILI: Naenda home mana nitawezaje kufanya kazi na giza?...
.
Bosi alichoka mana akaona bora wa kwanza kuliko huyu wa pili! Eti Yule wakwanza ndio alikuwa taa sasa kama anaondoka basi ofisini patakuwa giza……

No comments:

Post a Comment