Happines Watimanywa Redd's Miss Tanzania 2013.
Mkoa wa Dodoma
hapo jana uliibuka kidedea katika kinyang’anyiro cha Redd’s Miss
Tanzania 2013
kupitia Mrembo wake Happiness Watimanywa baada ya kuwapiku warembo
wengine kutoka vitongoji na mikoa mbalimbali Nchini Tanzania.
Watimanywa
mbali ya kuchukua Taji la Redd’s Miss Tanzania, pia aliweza kushinda kama Miss
Photogenic ambapo ilimuwezesha kuingia
Tano bora pamoja na wenzie wanne walioshinda mataji mbalimbali kama vile Nalietha Boniface (Miss Temeke) aliechukua Taji la Miss Top Modal, Prisca Clement (Miss Sinza) Taji Miss Talent, Clara Bayo (Miss Dar City Center) Taji Miss Top sports woman na Severina Lwinga(Miss Highland) Taji Miss Personality.

Vilevile, Happiness Watimanywa ana shahada ya
kwanza ya Biashara aliyoipata chuo cha
Strathclyde University cha Uingereza na aliwahi kuwa wa kwanza na kuongoza nchi
zipatazo 150 katika somo la Accounts kwa shule zinazofanya mtandao wa IGCSE. Pamoja na kushinda taji la Miss Tanzania jana, alikuwa ni Miss Dodoma 2013 na
Miss Kanda ya Kati 2013 ambapo pamoja na kuwa Miss Tanzania bado anayashikilia
mataji hayo mpaka mwakani.
Redd’s Miss Tanzania mwaka huu Happiness Watimanywa(kati) akiwa katika picha ya pamoja na washindi wenzie. Kutoka kushoto ni mshindi wa
pili Latifa Mohamed, Tatu ni Clara Bayo(kulia).
No comments:
Post a Comment