Kijana
Hassan Omary mkazi wa Buguruni amejikuta akienda jela miezi sita baada ya
kujisaidia haja kubwa na ndogo Mahamani, mbele ya Hakimu Mfawidhi William
Mutaki wakati akisomewa shitaka lake la uzururaji.
Kitendo
hiki kilitokea Juma tano iliopita Mahama ya Jiji ilioko Sokoine Drive Jijini
Dar wakati Mwendesha mashitaka, Richard Magodi akimsomea Mtuhumiwa shitaka la
kuzurura hovyo. Kipindi wakisubiria Bw.Omary kukiri au kukanusha shitaka hilo cha
kushangaza hakujibu kitu nakubaki akiwakodolea macho waendesha mashitaka
waliopo Mahakamani hapo.
Ghafla,
Mtuhumiwa alionekana akijikamua kama mtu ambae anataka kujisaidia na ndipo
ilipoanza kusikika halafu mbaya ya kinyesi iliotapakaa Mahamani hapo na kusababisha
shughuli zote kusimama huku watu wote waliokuwepo eneo hilo kutoka nje wakiziba
pua zao akiwemo Hakimu aliekuwa akiendesha kesi.
Pamoja,
na hukumu hiyo alioipata Kijana Hassan, alijikuta akichapwa viboko kutoka kwa
askari waliokuwepo eneo hilo la Mahakama na kumlazimisha apige deki mikojo yake
na kuzoa kinyesi kilichochafua chumba cha Mahakamani hapo.
No comments:
Post a Comment