Sep 24, 2013

MSANII BLACK RHYNO APATA MTOTO WA KIKE



Msanii wa Hip hop nchini Tanzania ajulikanae kama Black Rhyno Mchana  huu amepata mtoto wa kike baada ya mkewe kujifungua salama katika hospital ya Muhimbili.

Rhyno ambae ni mdogo wa Mwanamuziki mkongwe wa kizazi kipya bongo, Profesa Jay amesema hayo leo katika Mtandao wa kijamii, na kumshukuru mungu kwa kumsaidia mkewe kujifungua salama na anaiona hiyo ni kama zawadi kwake.

“Mwenyezi Mungu amenibariki sana leo kwa kunipa zawadi kubwa ya mtoto na kumfanya mke wangu kujifungua salama katika hospital ya Muhimbili Mchana wa saa saba na nusu”. Amesema Rhyno

Rhyno kwa sasa anatamba na ngoma zake kama “Taking over na Mke Mwema” ambazo zote amemshirikisha Soprano.
                      Black Rhyno akiwa na Mkewe kabla ya kujifungua

No comments:

Post a Comment