Msemaji wa Al-Shabaab Ali Mohamud Rage
Mwandishi wa Channel
4 News Jamal Osman
Taarifa hii imepatikana pale Mwandishi wa Habari wa Channel
4 News Jamal Osman
kufanya mahojiano na Msemaji wa Al-Shabaab kujua sababu iliowapelekea
kuvamia jengo la Biashara lijulikano kama Westgate Nchini Kenya na kuua watu
wapatao 69, Majeruhi 175 na Mateka kadhaa kutoka Nchi mbalimbali waliokuwemo
eneo hilo.
Haya ndio mahojiano yao yalioko katika tafsiri ya Kiswahili.
Jamal Osman: Kwanini mmefanya shambulio?
Msemaji wa Al-Shabaab: Sababu ya
kufanya shambulio ni kuwalinda watu wetu na nchi yetu sababu Kenya
ilitushambulia, bado wanaendelea kushikilia sehemu ya ardhi yetu. Tumekuwa
majirani wenye amani, lakini wao ndio walitushambulia na tunajilinda.
Haijalishi kama wewe ni Muislamu ama Mkristo, sheria inasema unatakiwa
kujilinda mwenyewe dhidi ya yule aliyekushambulia.
Jamal Osman: Mmeua watu wa mataifa mengi
wakiwemo Waingereza, hamuogopi mataifa makubwa yatawatafuta?
Msemaji wa Al-Shabaab:
Tumewaambia Wakenya na wale wanaoenda Kenya kwamba hatuwezi kuvumilia kile Kenya
inatufanyia. Tuliwaambia tutajilinda wenyewe na tuliwaonya kuhusu kwenda Kenya.
Wakenya wana damu yetu mikononi mwao. Mtu yeyote aliyejiandaa kwenda Kenya
lazima ajiandae na kukabiliana na ukweli huo, na hatuwaogopi watu wa Ulaya ama
Wamarekani sababu sisi si wadhaifu. Na tunasema hili kwa watu wa Ulaya na
Wamarekani ambao wamekuwa wakiwasaidia wale wanaotushambulia, muwaambie Wakenya
waache uonevu wao kama mnataka kuwa salama.
Jamal Osman: Kwanini mliilenga mall ya Westgate?
Msemaji wa Al-Shabaab: Sababu ya
kwanini tuliilenga mall ya Westgate, ni kwakuwa Wakenya na serikali yao
wametumia majeshi dhidi yetu, ni maadui wetu. Wamewatuma watu wao Somalia,
wameiunga mkono serikali yao kuishambulia nchi yetu. Kwetu, popote pale Kenya
ni sawa, tutawapiga popote tuwezapo. Sababu tulilenga Westgate ni kwamba
tunajua ni sehemu ambayo wanajisikia maumivu zaidi. Ni kwasababu inaingiza hela
nyingi na ipo katikati ya jiji. Ni sehemu wanasikia maumivu na kwasababu
tulitaka kutuma ujumbe na hatukutaka kuupoteza ujumbe wetu. Tulitaka ujumbe
wetu umfikia kile Mkenya.
Jamal Osman: Wapiganaji wenu ndani ya mall bado
wanapigana?
Msemaji: Ni zaidi ya saa 27 sasa, wapo ndani na bado wameshika hatamu.
Msemaji: Ni zaidi ya saa 27 sasa, wapo ndani na bado wameshika hatamu.
Westgate Mall kabla ya tukio
Jamal Osman: Nasikia kuna mpiganaji mwanamke
ndani pia?
Msemaji: Hatupeleki wanawake wetu kwenye
uwanja wa vita.
Jamal Osman: Kitu gani mnategemea kitatokea
sasa? Nini litakuwa tokeo la hili?
Msemaji: Kama Mungu akipenda, tunategemea
Wakenya watapata ujumbe kwamba kama ukimwaga damu, damu yako itamwagika pia.
Kwao kujua kuwa hawawezi kushikilia Kismayu, Dhobley na Afmadow na wategemee
waishi kwa amani Nairobi. Huo ni ujumbe tunataka kuutuma kwao.
Jamal Osman. Kwenye jumbe zenu kupitia Twitter
mnasema huu ni mwanzo tu na mtaendelea, ama mmeshafikia malengo yenu?
Msemaji: Tunasema kwa Kenya, iacheni nchi
yetu. Huo ni ujumbe wa kwanza. Na kama wakikataa kuiacha nchi yetu basi
tutaanzisha vita yenyewe.
Jamal Osman: Hivyo matakwa yenu kwa Wakenya, ni
kuiacha nchi yenu kama wanataka amani?
Msemaji: Kama Wakenya wanataka amani, wanatakiwa kuiacha nchi yetu.
Msemaji: Kama Wakenya wanataka amani, wanatakiwa kuiacha nchi yetu.
Jamal Osman: Kwanini mnawalenga watu wasio na
hatia?
Msemaji: Raia wa kigeni, wanatakiwa kuondoka
kwenye nchi hiyo (Kenya) kwasababu Wakenya na Al-Shabaab wapo kwenye mgogoro na
tunamwambia kila mtu – Kenya ni eneo la vita.
Jamal Osman: Kwakuwa unasema raia wa kigeni na
Waingereza wana maslahi makubwa nchini Kenya, mna ujumbe gani kwao?
Msemaji: Tunasema kwa Waingereza, kwakuwa
tunaamini wanawasaidia Wakenyan na Wakenya ni watumwa wao, hivyo wanatakiwa
kuwaambia Wakenya, walitoe jeshi lao Somalia. Na Waingereza wanajua Wasomali
hawataka tamaa. Tuliwakatalia Waingereza mwanzoni, ambao wana nguvu kuliko
Wakenya.
waaapi, dua la kuku hilo wanamjua mmarekani au wanamuona kwenye Tv tu? wamuulize Osama & Sadam!!
ReplyDelete