Sep 26, 2013

MTOTO WA GENERALI WA JESHI NCHINI CHINA AENDA JELA MIAKA 10 KWA UBAKAJI.


Li Tianyi(17) 

Mahakama ya Haidian Kaskazini Magharibi mwa Beijing, imemuhukumu miaka 10 kwenda gerezani mtoto wa mmoja wa Majenerali wakuu wa Jeshi la China ajulikanae kama Li Tianyi(17) kwa kosa la ubakaji alilofanya mwezi Februari akiwa na wenzie wanne.

Kwa mujibu wa “Bbc Swahili” inasema kuwa, kijana huyu sio mara ya kwanza kuhusika katika tukio ambalo limeghadhabisha umma. Kwani mara kwa mara amekuwa ni kijana mkolofi sana mpaka kupelekea kuchukiwa na wakazi wa Nchi hiyo.

Kama vile mnamo mwaka 2011, aliweza kuzuiliwa kwa mwaka mmoja baada ya tukio moja la barabarani alipokuwa anaendesha gari ambalo halikuwa na nambari ya usajili, pamoja na kuwatolea maneno machafu mtu na mkewe waliokuwa ndani ya gari lao na kupelekea umma kushangazwa na tabia yake hiyo.

Inasemekana kuwa  ni desturi kwa watoto wa watu mashuhuri nchini china kuvunja sheria hadi kuzalisha hasira miongoni mwa watu wanaowaona ni kama wasio na maadili na wenye kuhujumu sheria.

No comments:

Post a Comment