Watu sita wafariki dunia kwa ajali Roli ambalo
lilikuwa limebeba mbao kutokea mkoani Iringa na kupinduka mkoani Manyara maeneo
ya Babati leo Asubuhi.
May 25, 2012
MBUNGE WA ROMBO MH. JOSEPH SELASINI AMPOTEZA MAMA YAKE KATIKA AJALI JANA
Mbunge wa Rombo Mheshimiwa Joseph Selasini (CHADEMA) amempoteza
mama yake mzazi katika ajali ya gari
iliotokea jana katika eneo la Boma Ng'ombe wilayani Hai mkoani Kilimanjaro,
alipokuwa safarini kutoka Arusha akiwa na familia yake.
May 21, 2012
WANAFUNZI WA SHAHADA YA HABARI SAUT WATENGENEZA MAKALA YA KUMBUKUMBU YA MV BUKOBA HII HAPA
Leo ni siku ya kumbukumbu ya ajali ya meli MV BUKOBA iliotokea May 21,1996 katika ziwa victoria na kuuwa watu wengi sana.
Kupitia ajali hii wanafunzi wa mawasiliano ya Umma na uwandishi wa habari wa chuo kikuu cha Mt. Augustino Mwanza chini ya usimamizi wa Mhadhili wao Bw.Robert Mkosamali wameweza kuandaa MAKALA FUPI ya ajali hii sikiliza hapo chini.
UTUPWAJI MBAYA WA KONDOM WALETA MAJONZI KWA WAKAZI MWANZA
Utupwaji ovyo wa kondom zilizotumika umekithili jijini mwanza ambapo watu wengi wamekuwa wakilalamika kutokana na kitendo hicho kimekuwa ni hatari kwa afya za wakazi wa maeneo yao hasa watoto wanapozikuta zimetupwa na kuzichukua kwa kuwa wengi wao hawajui madhara yake.
May 18, 2012
RADIO SAUT FM MWANZA YATIMIZA MIAKA 14 TOKEA KUANZISHWA KWAKE
Watangazaji na wafanyakazi wa radio SAUT FM iliopo Mwanza wanayofuraha ya
kuwakaribisha wadau na wapenzi wao katika maadhimisho ya kuzaliwa kwa radio hiyo
inayotimiza miaka 14 tokea kuanzishwa kwake
itakayo fanyika kesho Juma mosi kuanzia saa 1 usiku hadi majogoo katika
viwanja vya Raila Odinga viliopo katika chuo kikukuu cha Mt. Augustino jijini Mwanza.
Subscribe to:
Posts (Atom)


