Feb 1, 2014

NASH Mc : USHIKAJI NA UMKOA KATIKA BAADHI YA RADIO ZA BONGO USHUSHA NA KUPOTEZA VIPAJI VYA WANAMZIKI WA KIZAZI KIPYA.

Haya yamesemwa leo na Mwana Hip Hop wa Kitanzania ajulikanae kama NASH Mc alipokuwa akiojiwa katika kipindi cha Planet Bongo cha East Afrika Radio.

Akuishia hapo lakini ametolea ufafanuzi kwa yale yote alioyaongelea katika Mahojiano hayo katika akaunt yake ya Facebook kama ifuatavyo.

Oct 13, 2013

SABABU ZA MTANGAZAJI WA ITV UFOO SARO KUPOTEZA MAMA NA YEYE KUPIGWA RISASI LEO HIZI HAPA



Mtangazaji wa ITV ajulikanae kwa  jina  la  Ufoo Saro  amejeruhiwa  vibaya  kwa  kupigwa  risasi  na  mchumba  wake ambaye pia alimuu na mama mkwe wake kisha naye alijipiga risasi na kujiua Alfajiri  ya  leo.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa kipolisi wa Kinondoni kamanda Wambura  amethibitisha tukio hilo alipoongea na Radio One nakusema kuwa Ufoo alipigwa risasi na mchumba wake ambae anafanya kazi  katika umoja wa mataifa ( UN ) huko Sudani ila bado haijafahamika  kitengo alichokuwa  akifanyia  kazi.

Oct 12, 2013

KING MAJUTO NA UBUNGE MWAKA 2015

Mchekeshaji mkongwe nchini Tanzania King Majuto (65) anategemea kugombea ubunge ifikapo mwaka 2015 katika uchaguzi mkuu kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi(CCM).

Majuto amesema kuwa, Mungu akimjalia afya njema kuufikia kipindi icho basi atagombea ubunge katika jimbo lake la Tanga Mjini, lakini ikishindikana atagombea kwenye wilaya ya Mkinga kwani analifahamu vizuri jimbo hilo na matatizo yanayowakabili wakazi wake.

Oct 11, 2013

MSANII LISSA WA VITUKO SHOW AWAOMBA RADHI MAFANS JUU YA PICHA ZAKE ZA UTUPU KUVUJA MITANDAONI


Baada ya Msanii wa Vichakesho(Comedy) LIssa Mlaki wa kundi la Vituko Show linalorusha kazi zake Channel Ten  picha zake za utupu kuvuja mitandaoni bila mapenzi yake, ameonekana kupata shida sana kutoka kwa mashabiki wake.

Jicho Lako.com tulipoongea nae ameonekana kushangazwa sana baada ya kuziona picha hizo ambazo amekubali ni zake ingawa amesema hakuzipiga kwa lengo baya kama inavyoongelewa mitandaoni.

 “Sijafanya kusudi bhana ilikuwa tunapigana picha hapa kambini siunajua tena mambo ya waschana  ingawa bado sijamjua ni nani kati yetu hapa kambini ameamua kanichezea mchezo mchafu wa kuzisambaza mitandaoni”. Amesema Lissa

Ameongeza kwa kusema alikuwa hajui chochote kwani walipokuwa wanapiga picha hizo ilikuwa nikatika kujifurahisha wao wenyewe na wasichana wenzake hapo kambini wala sio njia ya kutaka kujulikana kama watu wengine wanavyosema au wanaondelea kucomment katika mitandao ya kijamii na blogs.

Lakini pia imeonekana kama ni kutaka kunichafua tu mana kuna picha zangu nakubali lakini nyingine sio zangu ingawa wamezionganisha ili zionekane zote zangu. Hivyo bado nakifuatilia hapa kambini chanzo kilichosambaza picha zangu najua atakuwa mmoja wa wasichana tuliokuwa nao. Lissa amesema
Lissa(Kulia) akiwa pamoja na Msanii mwenzio Kinyambe(Kushoto)
 
Pamoja na hayo, Lissa amewaomba radhi ya dhati kabisa Watanzania na Mashabiki zake wote wamsamehe kwa hili kwani halikuwa lengo lake la kupiga picha hizo na kuzitupia Mitandaoni kama inavyonekana kwa sasa kwani imetokea kumchanganya na kumsumbua sana. Kutokana kuwa tokea picha hizo zionekane mitandaoni simu yake imekuwa ikipigwa sana kwa kumlaumu na wengine kukoment vibaya katika picha zake hata kama ni zakwaida anazozipost katika Mtandao wa kijamii wa Facebook.

Kwa wale wasiomjua labda kwa Jina hili ila ni yule Mdada ambae upenda kuigiza kama Mchaga na ndio stlye inayompa umaarufu kila iitwapo leo. Tumeona Wasnii wengi wa Comedy Nchini utumia style mbalimbali za uigizaji kama vile ukimcheki Kitale na style ya Uteja na wengine wengi

WAZIRI NCHIMBI AUNDA KIKOSI KAZI CHA KUZUIA MAUAJI YA VIKONGWE NCHINI(PATA BARUA HUSIKIA KWA VYOMBO VYA HABARI HAPA)