Oct 13, 2013

SABABU ZA MTANGAZAJI WA ITV UFOO SARO KUPOTEZA MAMA NA YEYE KUPIGWA RISASI LEO HIZI HAPA



Mtangazaji wa ITV ajulikanae kwa  jina  la  Ufoo Saro  amejeruhiwa  vibaya  kwa  kupigwa  risasi  na  mchumba  wake ambaye pia alimuu na mama mkwe wake kisha naye alijipiga risasi na kujiua Alfajiri  ya  leo.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa kipolisi wa Kinondoni kamanda Wambura  amethibitisha tukio hilo alipoongea na Radio One nakusema kuwa Ufoo alipigwa risasi na mchumba wake ambae anafanya kazi  katika umoja wa mataifa ( UN ) huko Sudani ila bado haijafahamika  kitengo alichokuwa  akifanyia  kazi.

Oct 12, 2013

KING MAJUTO NA UBUNGE MWAKA 2015

Mchekeshaji mkongwe nchini Tanzania King Majuto (65) anategemea kugombea ubunge ifikapo mwaka 2015 katika uchaguzi mkuu kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi(CCM).

Majuto amesema kuwa, Mungu akimjalia afya njema kuufikia kipindi icho basi atagombea ubunge katika jimbo lake la Tanga Mjini, lakini ikishindikana atagombea kwenye wilaya ya Mkinga kwani analifahamu vizuri jimbo hilo na matatizo yanayowakabili wakazi wake.

Oct 11, 2013

MSANII LISSA WA VITUKO SHOW AWAOMBA RADHI MAFANS JUU YA PICHA ZAKE ZA UTUPU KUVUJA MITANDAONI


Baada ya Msanii wa Vichakesho(Comedy) LIssa Mlaki wa kundi la Vituko Show linalorusha kazi zake Channel Ten  picha zake za utupu kuvuja mitandaoni bila mapenzi yake, ameonekana kupata shida sana kutoka kwa mashabiki wake.

Jicho Lako.com tulipoongea nae ameonekana kushangazwa sana baada ya kuziona picha hizo ambazo amekubali ni zake ingawa amesema hakuzipiga kwa lengo baya kama inavyoongelewa mitandaoni.

 “Sijafanya kusudi bhana ilikuwa tunapigana picha hapa kambini siunajua tena mambo ya waschana  ingawa bado sijamjua ni nani kati yetu hapa kambini ameamua kanichezea mchezo mchafu wa kuzisambaza mitandaoni”. Amesema Lissa

Ameongeza kwa kusema alikuwa hajui chochote kwani walipokuwa wanapiga picha hizo ilikuwa nikatika kujifurahisha wao wenyewe na wasichana wenzake hapo kambini wala sio njia ya kutaka kujulikana kama watu wengine wanavyosema au wanaondelea kucomment katika mitandao ya kijamii na blogs.

Lakini pia imeonekana kama ni kutaka kunichafua tu mana kuna picha zangu nakubali lakini nyingine sio zangu ingawa wamezionganisha ili zionekane zote zangu. Hivyo bado nakifuatilia hapa kambini chanzo kilichosambaza picha zangu najua atakuwa mmoja wa wasichana tuliokuwa nao. Lissa amesema
Lissa(Kulia) akiwa pamoja na Msanii mwenzio Kinyambe(Kushoto)
 
Pamoja na hayo, Lissa amewaomba radhi ya dhati kabisa Watanzania na Mashabiki zake wote wamsamehe kwa hili kwani halikuwa lengo lake la kupiga picha hizo na kuzitupia Mitandaoni kama inavyonekana kwa sasa kwani imetokea kumchanganya na kumsumbua sana. Kutokana kuwa tokea picha hizo zionekane mitandaoni simu yake imekuwa ikipigwa sana kwa kumlaumu na wengine kukoment vibaya katika picha zake hata kama ni zakwaida anazozipost katika Mtandao wa kijamii wa Facebook.

Kwa wale wasiomjua labda kwa Jina hili ila ni yule Mdada ambae upenda kuigiza kama Mchaga na ndio stlye inayompa umaarufu kila iitwapo leo. Tumeona Wasnii wengi wa Comedy Nchini utumia style mbalimbali za uigizaji kama vile ukimcheki Kitale na style ya Uteja na wengine wengi

WAZIRI NCHIMBI AUNDA KIKOSI KAZI CHA KUZUIA MAUAJI YA VIKONGWE NCHINI(PATA BARUA HUSIKIA KWA VYOMBO VYA HABARI HAPA)


Oct 7, 2013

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI YANYAKUA VIKOMBE VITATU NA MEDALI TATU SHIMIWI DODOMA



Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (watatu kushoto) akimpongeza mchezaji wa riadha wa Mambo ya Ndani Sports Klabu baada ya kumvisha medali mchezaji huyo katika hafla ya kufunga Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara  za Serikali (SHIMIWI),  yaliyomalizika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).




Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi (kushoto) akimkabidhi kikombe cha ushindi  Kapteni wa timu ya Kuvuta Kamba Wanaume ya Mambo ya Ndani Sports Klabu baada ya timu hiyo kuibuka mshindi wa pili katika Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara  za Serikali (SHIMIWI), yaliyomalizika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

Oct 6, 2013

UNHCR YAIOMBA RADHI SERIKALI YA TANZANIA JUU YA SWALA LA WAKIMBIZI




JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI



Simu:  +255-22-2112035/40
S.L.P.  9223
Nukushi:  +255-2122617/2120486
Barua Pepe:  ps@moha.go.tz
Dar es Salaam


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), limeiomba radhi Serikali ya Tanzania kufuatia taarifa waliyoitoa kwenye Mkutano wa 64 wa Kamati Tendaji (EXCOM) ya shirika hilo uliofanyika Geneva, Uswisi tarehe 30 Septemba hadi tarehe 4 Oktoba, 2013. Katika taarifa yao kuhusu Afrika, UNHCR ilieleza kuwa Tanzania imewafukuza Wakimbizi wa Rwanda na Burundi katika operesheni ya kuwaondoa Wahamiaji haramu inayoendelea nchini.

UNHRC imeiomba radhi Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia barua yake ya tarehe 2 Oktoba, 2013. Barua hiyo imeandikwa na Mkurugenzi wa UNHCR Kanda ya Afrika Bw. George Okoth-Obbo kwenda kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Ame Silima  aliyeongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo unaofanyika kila mwaka.
Katika barua hiyo, UNHCR imeeleza kusikitishwa na taarifa hiyo ambayo si ya kweli na imekiri kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikishirikiana kwa karibu na UNHRC katika ngazi zote kuhakikisha kwamba hakuna mkimbizi anayerejeshwa kwao katika zoezi la kuwakamata na kuwarejesha kwao wahamiaji haramu linaloendelea nchini Tanzania.

Aidha, Bw. Okoth Obbo ameeleza kuwa UNHCR  na Jumuiya ya Kimataifa kwa ujumla inatambua na kuthamini kwa dhati mchango mkubwa ambao Tanzania imeutoa na inaendelea kuutoa katika kuwahifadhi wakimbizi wa mataifa mbalimbali kwa kipindi cha takribani miaka 40.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea kauli hiyo na kueleza kwamba inatarajia na inaamini kwamba UNHCR itaendelea kutoa taarifa sahihi zenye kutoa picha halisi inayoonesha namna Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyotekeleza wajibu wake  kuwalinda na kuwahifadhi Wakimbizi kwa mujibu wa Sheria za nchi na mikataba ya Kimataifa ambayo nchi imeridhia.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
06, Oktoba, 2013







Oct 4, 2013

BALOZI WA UHOLANZI NCHINI, AMTEMBELEA WAZIRI DK. EMMANUEL NCHIMBI OFISINI KWAKE, DAR ES SALAAM LEO.



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) akizungumza na Balozi wa Uholanzi nchini, Jaap Frederiks masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Uholanzi. Balozi huyo alimuhakikishia Dk Nchimbi ushirikiano wa hali ya juu kati ya nchi yake na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika ofisini kwa Waziri Nchimbi, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) akimsikiliza kwa makini Balozi wa Uholanzi nchini, Jaap Frederiks wakati walipokuwa wanajadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya yake na Tanzania. Balozi huyo alimtembelea Waziri Nchimbi ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) akimshukuru Balozi wa Uholanzi nchini, Jaap Frederiks kwa kumtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo kwa lengo ya kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya wizara yake na Nchi ya Uholanzi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.