Sep 23, 2013

AL-SHABAAB YAWATAADHARISHA WAGENI KUINGIA NCHINI KENYA

Msemaji wa Al-Shabaab Ali Mohamud Rage
Mwandishi wa Channel 4 News Jamal Osman  
 
Taarifa hii imepatikana pale Mwandishi wa Habari wa Channel 4 News Jamal Osman

Sep 22, 2013

DODOMA YALA BINGO REDD’S MISS TANZANIA 2013

Happines Watimanywa Redd's Miss Tanzania 2013.

Mkoa wa Dodoma hapo jana uliibuka kidedea katika kinyang’anyiro cha Redd’s Miss Tanzania 2013 
kupitia Mrembo wake Happiness Watimanywa baada ya kuwapiku warembo wengine kutoka vitongoji na mikoa mbalimbali Nchini Tanzania.

Watimanywa mbali ya kuchukua Taji la Redd’s Miss Tanzania, pia aliweza kushinda kama Miss Photogenic ambapo ilimuwezesha kuingia

Sep 21, 2013

APIGWA MIEZI SITA JELA KWA KOSA LA KUJISAIDIA MAHAKAMANI



Kijana Hassan Omary mkazi wa Buguruni amejikuta akienda jela miezi sita baada ya kujisaidia haja kubwa na ndogo Mahamani, mbele ya Hakimu Mfawidhi William Mutaki wakati akisomewa shitaka lake la uzururaji.

Kitendo hiki kilitokea Juma tano iliopita Mahama ya Jiji ilioko Sokoine Drive Jijini Dar wakati Mwendesha mashitaka, Richard Magodi akimsomea Mtuhumiwa shitaka la kuzurura hovyo. Kipindi wakisubiria Bw.Omary kukiri au kukanusha shitaka hilo cha kushangaza hakujibu kitu nakubaki akiwakodolea macho waendesha mashitaka waliopo Mahakamani hapo.


Ghafla, Mtuhumiwa alionekana akijikamua kama mtu ambae anataka kujisaidia na ndipo ilipoanza kusikika halafu mbaya ya kinyesi iliotapakaa Mahamani hapo na kusababisha shughuli zote kusimama huku watu wote waliokuwepo eneo hilo kutoka nje wakiziba pua zao akiwemo Hakimu aliekuwa akiendesha kesi.

Pamoja, na hukumu hiyo alioipata Kijana Hassan, alijikuta akichapwa viboko kutoka kwa askari waliokuwepo eneo hilo la Mahakama na kumlazimisha apige deki mikojo yake na kuzoa kinyesi kilichochafua chumba cha Mahakamani hapo.

Chanzo: Vituko vya Mtaa

Sep 20, 2013

KUMBE HUYU NDIO CHANZO CHA UMASIKINI WA WASANII WA FILAM NCHINI

William Mtitu

Inajulikana kuwa Wasanii wetu wanaigiza Filam nyingi sana lakini mwisho wa siku ukijakufuatilia maisha yao kiundani au wakifariki utagundua siri kubwa sana iliojificha hasa pale utakapogundua kuwa Msanii ameondoka hana Nyumba wala Biashara ya maana inayoendana na umaarufu alionao.
Kwa mujibu wa Wiliam Mtitu ambae anamiliki kampuni ya Filamu ijulikanayo kama 5Effects, amesema kwa kiasi kikubwa  Wasambazaji wa kazi zao ndio chanzo kikubwa cha wao kuwa au kufa wakiwa masikini pamoja na kufanya kazi nyingi sana ambazo kwa uhalisia wake lazima zingemfanya mtu awe na maisha mazuri.
Amesema haya pale alipopost kwenye mtandao wa kijamii kuwa “BILA STEPS

Sep 17, 2013

DAYNA KUTOKA MUZIKI HADI UWANAMITINDO

Mwanamuziki wa kizazi kipya Dayna Nyange a.k.a Dayna kuingia katika mitindo kutokana na chanzo hiki EJ FASHION & MEDIA.Dayna amedai yakuwa hivi karibuni ataingia kwenye tasnia ya fashion akiwa kama mwanamitindo au mbunifu wa mavazi.

Hii imetokana baada ya kuonekana mara nyingi akiwa karibu na mwana mitindo maarufu jokate Mwegelo kwa kuwa ndio rolemodel wake katika mitindo.

Pamoja na hayo, inaonekana katika kubadilishana fani au kuonesha vibaji walivyonavyo wadada hawa kutokana kuwa hivi karibuni nae Jokate ameonekana kuingia katika muziki hasa baada ya kutoa ngoma alioshirikiana na Lucci inayoenda kwa jina la Dada & Kaka
 Dayna Nyange
Dayna & Jokate