Apr 13, 2012

BABA LULU AMEIOMBA JAMII HISIMUHUKUMU MWANAE


BABA mzazi wa msanii wa filamu, ELIZABETH MICHAEL (LULU) ameiomba jamii ya Tanzania kutomhukumu mwanae kutokana na kifo cha marehemu STEVEN KANUMBA, badala yake iache vyombo vya sheria vifanye kazi yake.

Mzazi huyo, MICHAEL EDWARD KIMEMETA (49) mzaliwa wa Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, amewaomba Watanzania kuiachia Mahakama iamue kama mtoto wao anahusika katika kifo hicho ama la, na ameongeza kuwa binti yake ana umri wa miaka 16 kutokana alizaliwa April 17,1995 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam tofauti na inavyoelezwa kuwa ana miaka 18.

Pamoja na hayo Kumekuwa na utata uliojitokeza kuhusu umri wa Lulu . Wakati mwenyewe akieleza kuwa ana miaka 17, Jeshi la Polisi lilieleza kuwa umri wake ni miaka 18 na juzi Mahakama iliambiwa kuwa msanii huyo ana umri wa miaka 17.

No comments:

Post a Comment