Kutokana na
watu wengi kuuliza juu ya ratiba nzima ya mazishi ya aliekuwa icon wa movie
Tanzania Steven Kanumba sasa hii ni ratiba yenyewe.
Mwili wa
marehemu Steven Kanumba utachukuliwa kwa msafara kutoka Hospitali ya Taifa,
Muhimbili saa 2:30 asubuhi. Utapitishwa Barabara ya Umoja wa Mataifa na Ali
Hassan Mwinyi hadi Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni ambako Misa ya kumuombea
itasomwa pamoja na salamu mbalimbali kabla ya watu wote kumuaga.
Wito unatolewa kwa watu kujitokeza kwa wingi kuanzia saa 2:00 asubuhi, wakijipanga kando ya Barabara za Umoja wa Mataifa na Ali Hassan Mwinyi ili wautolee heshima mwili wa Kanumba wakati ukitolewa Muhimbili kwenda Leaders Club.
Saa 3:30
asubuhi, mwili wa Kanumba utapokelewa Viwanja vya Leaders, ukitanguliwa na
mapokezi ya wazazi wake, viongozi mbalimbali wa serikali ambao juu yao kabisa
atakuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Gharib
Bilal.
Saa 4:00,
itakuwa ni muda wa kusoma Misa ambayo itachukua dakika 60, saa 5:00 kitakuwa
kipindi cha salamu kutoka kwa watu mbalimbali.
Saa 6:00
mchana, ratiba ya kumuaga Kanumba itaanza mpaka saa 9:00 alasiri na baada ya
hapo, utakuwa wakati wa kuusafirisha mwili kwa msafara kutoka Leaders Club
mpaka Makaburi ya Kinondoni, msafara ukipita Barabara ya Tunisia, utakatisha
Barabara ya Kinondoni kuelekea makaburini.
Saa 10:00
alasiri, mazishi yatafanyika kwa kufuata utaratibu wa imani ya marehemu.
Kamati ya
Mazishi inatoa wito kwa watu watakaohudhuria shughuli ya kumzika ndugu yetu
Kanumba, kuja na maua ili kumuaga kwa heshima.
Utulivu,
unyenyekevu na ustahimilivu ni mambo muhimu yanayohitajika katika kipindi chote
cha kumuaga mpendwa wetu Kanumba.
Mungu
ailaze roho ya Kanumba mahari pema peponi Amen……
K.N.Y GABRIEL MTITU
MWENYEKITI WA KAMATI YA MAZISHI
No comments:
Post a Comment