Waziri mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda amekanusha kuwa kuna mawziri nchini wamejiuzuru kutokana na shinikizo la baadhi ya wabunge wa bunge la jamuhuru ya muungano wa Tanzania.
Amesema hayo leo alipokutana na waandishi wa habari bungeni mkoani Dodoma na kumwambia kuwa kuna taarifa zimetoka gazetini zinazosema kuwa takribani mawaziri wa nane wamejiuzuru nyazifa zao.
Pinda amesema kuwa huo ni uvumi tu wa viombo vya habari kwasababu yeye ajathibitisha hilo kutokana hajapata kusoma hilo gazeti lililotoa habari hizo na wala hadi muda huu hajapata barua za kujiuzuru kutoka kwa mawaziri hao.
Ameongeza kuwa kama hizo taarifa ni za kweli basi ni vyema watu wakasubiri hadi juma tatu ndio jibu sahihi litatoka lakini kwa sasa ni haraka mno kwa sababu yeye hana taarifa hivyo awezi sema kitu juu ya hilo hadi atakapokuja kulithiitisha mwenyewe.
No comments:
Post a Comment