Tume ya kushughulikia Katiba Mpya ndio hiyo imeshateuliwa na Rais wetu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania sasa ni jukumu letu waandishi wa habari pamoja na wasomi hapa nchini kuelimishana sisi kwa sisi ili basi tunapoenda kufanya mchakato huu tuweze pata kile kilichobora kwetu na kizazi kunachokuja.
Swala la Katiba sio dogo kama tunavyolifikilia jamani hivyo ni vyema tukajua kwanza Katiba ni nini? kabla hatujaamua kitu gani kiweze kuwepo ndani yake, tunajua katiba ya zamani inamapungufu sasa inatubidi tujue mapungufu hayo na tuyalekebishe kwa kuweka mambo yatakayotufanya wananchi pamoja na serikali kuwa na mtazamo sawa wa mambo kwa maendeleo ya nchi yetu.
Nchi nyingi zilizoendelea kama Marekani, Ujerumani Afrika ya kusini na Uingereza zinakatiba zinazotoa usawa kwa raia na viongozi wake, hivyo basi ni vyema wananchi tukawa waangalifu tunapokwenda kwenye mchato huu kwa kuwa na msimamo wa kweli bila kudanganyika na kitu chochote kwani tujue tukikosea katika hili tutakuwa tumeharibu maisha yetu yote na ya kizazi kinachokuja kwa kupenda pesa zaidi kuliko ubinadamu.
Ninasema hivi kwasababu kunawatu kupitia mchakato huu wataingiza interesti zao binafsi na kuacha za jamii nzima kwa manufaa yao na familia zao. kwa mfano ebu tuangalie maisha ya ndugu zetu wanaoishi vijijini maisha yao yanatia huruma sana kutokana baadhi ya viongozi wetu hawaajiki kikweli na kuwa wazarendo wa nchi yao.
Mimi naona vijana na wasomi ndio tunajukumu kubwa sana la kutatua tatizo hili na kuisaidia jamii yetu hasa ya kijijini ndio inayotumiwa sana na watu wachache kwa kuwarubuni ili basi wawezekufanya kile wanachopenda wao na mwisho wake wanaachwa na mateso mengi kwa nyanja zote za kiafya, kielimu pamoja na kiuchumi.
Hivyo basi inatupasa kuitaji katiba amabayo itatupa uhuru wa kweli na sio wa maneno tu, hii ni kama vile kiongozi anapoonekana anamapungufu au makosa ya kisheria ni lazima awajibishwe kila mtu akiona, pia wananchi wawe na mamlaka ya kujua kila kitu kuhusu matumizi ya fedha zinazotumika yaani serikali iwe wazi bila kuwa na kificho chochote kile, najua serikali yetu ni safi kwani tumeona viongozi wengi wanajihuzuru na wengine kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Kwa kumalizia tu kwani nina maneno mengi yakuieleza jamii yetu lakini cha msingi wananchi tuwemakini sana katika swala hili narudia tena ni zito na la maisha yetu sio jambo la mchezo na ikiwezekana tutumie katiba au hatua za wenzetu kama Marekani, Ujerumani kwa nini wameendelea sisi kila siku tunaitwa nchi inayoendela? wakati china leo hii inaongoza duniani wakati mwanzo tulikuwa nao sawa? angalia Afrika ya kusini ni nchi iliopo Afrika kwa nini wao wameendelea wakati wote tupo bara moja? tuamke watamzania wenzangu tusiwejamvi la wageni.
Ikiwezekana hata katika hii migodi yetu tuweze kuiongoza wenyewe tunufaike nayo na wala sio wageni amabao tunaona wanavyonufaika na sisi wenyeji tunakufa njaa kila siku.
No comments:
Post a Comment