Oct 13, 2012

BAADHI YA PICHA NA TAARIFA JUU YA TUKIO LA JANA LINALOWAHUSU WAUMINI WA KIISILAMU KUCHOMA MOTO MAKANISA JIJINI DAR ES SALAAM











Vurugu kubwa zilizuka hapo jana asubuhi maeneo ya Mbagala Kizuiani jijini Dar es salaam baada ya Waumini wa Kiisilamu kuchukizwa na kitendo cha mtoto Emanuel Josephat(14) ambae ni Mkristo kukojolea kitabu cha Quraan, swala amabalo walidai ni kuidharau dini yao pamoja na kitabu hicho hivyo walikusanyika kituo cha polisi kilichopo maeneo hayo wakishinikiza wanamtaka mtoto huyo ili wamuue.

Waumini hao wanaokadiriwa kufikia idadi ya watu 3000 walitawanywa na  Polisi. Hivyo kutokana na kitendo hicho waliingia mitaani na kuchoma moto baadhi ya Makanisa na kuchukua vifaa vya muziki na kuviunguza hadharani pamoja na kusababisha gari za polisi namba T142 AVV,PT 0966 na T 325 BQP,basi la uda na gari la waandishi wa habari kutoka Clouds Media Group kuharibika kwa mawe ya waandamanaji hao.

Awali kabla ya tukio hilo Waumini wa dini ya Kiisilamu walikusanyika katika kituo hicho cha polisi wakimtaka mtoto huyo ambaye alikuwa chini ya ulinzi aachiwe na Polisi walipogoma kufanya hivyo ndipo vurugu hizo zilipoanza.

Kutokana na tukio hili kikosi cha kutuliza ghasia kilionekana kuzidiwa nguvu na watu hao ambao walikuwa wakiwatawanywa eneo moja  wanakimbilia eneo lingine na kuleta madhara mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufunga barabara.

Hatahivyo baada ya viongozi wa dini hiyo kufika wakiwa wameambatana na Sheikh wa Wilaya ya Temeke, Sheikh wa Taasisi na Jumuiya za Waislamu kukaa kikao na kamanda wa Polisi Wilaya ya Temeke, David Misime, walifikia muafaka wa kuwaita waislamu hao na kuwatuliza lakini hali iliendelea kuwa si shwari kwani baada ya viongozi hao kuona waandamanaji hao wakikamatwa na kupigwa walikuja juu na kutishia kuondoka.


No comments:

Post a Comment