Aliekuwa Msanii kutoka nchini Marekani Chauncey Hawkins ambaye wengi wanamjua kama Loon aliewahi kuwika katikati ya miaka ya tisini akiwa ni mmoja wa memba wa kundi la Bad Boy chini ya P Didy akiwa kama msanii, mtunzi na mwandishi wa wasanii wa kundi hilo amefungwa kwa kosa la usafirishaji wa madawa ya kulevya.
Huyu ni Loon wa sasa baada ya kubadili dini
Kwa mujibu wa Mtandao wa Bongo5 imepata nafasi ya kulonga na aliekuwa meneja wake ambaye pia alikuja naye hapa Tanzania mwaka 2006 na kuelezea nini kinaendelea kwa msanii huyo na wapi alipo kwa sasa na jina gani ambalo analitumia hasa baada ya kusilimu au kuwa muislam?
Meneja wa zamani wa msanii huyo amesema kwa sasa Loon yupo gerezani baada ya kukamatwa Novemba mwaka jana alipokuwa Ulaya nchini Belgium katika mhadhara na ndipo vyombo vya usalama vikamfungulia mashtaka yanayohusiana na kusafirisha ama kuuza unga unaotokana na safari zake za mara kwa mara nje ya Marekani mwaka 2006 hadi 2008.
Ameongeza kuwa Loon kwa sasa anajulikana kwa jina la Amir Junaid Muhadith na kwamba aliamua kusilimu bila kulazimishwa baada ya kufikiria sana namna maisha yake yalivyokuwa yanakwenda hasa pale alilipata nafasi ya kutembelea Dubai na kushangaa watu wote wakiacha kila kitu walichokuwa wanafanya na kukimbilia msikitini jambo ambalo lilimshtua sana kiasi cha kushangaa inakuwaje mji ambao una kila kitu kama wafanya biashara wakubwa, majengo mazuri na kila aina ya utajiri inapoita adhana basi kila kitu kinasimama kupisha swalaa halafu baada ya hapo watu wanarudi na kuendelea na mambo yao.
Nitofauti na Marekani amabayo ndio nchi yake pamoja na kuwa na wakristu wengi hakuna watu wanaoacha shughuli zao kama mikutano ya kibiashara, burudani na kisiasa kwa ajili dini yao kama alivyoshuhudia Dubai na ndipo alipo amua aanze kufuatilia kwa undani kuhusu Uislamu, na muktadha wake.
Aidha, Meneja huyo ameongeza tena kuwa Loon alipata upinzani mkubwa sana kutoka kwa familia yake na baadhi ya taasisi za kiusalama nchini Marekani juu ya uamuzi wake kwa kuanza kumchunguza pamoja na kuzuia passpoti yake mara kadhaa ili asisafiri kwenda ghuba ya uajemi ambapo ndipo wanaona palipokuwa kichocheo kikubwa kwa yeye kusilimu na kuchukua taadahari mana angeweza kuwashawishi wamarekani vijana kufuata njia yake.
Hivyo basi kutokana na kukamatwa kwake nchini Belgium Novemba 22 mwaka jana kumesababisha kuzuiwa kwa akaunti pamoja na mali zake zote, kabla ya kusafirishwa na kurudishwa Marekani mwezi wanne mwaka huu ambapo yupo katika gereza la New Hanover County Detention Center hadi sasa na kesi yake itaendelea kusikilizwa Mwezi Desemba mwaka huu baada ya kusogezwa mbele kutoka mwezi huu wa kumi.
No comments:
Post a Comment