Oct 26, 2012
MAJINA YA WALIOMUUA KAMANDA WA MKOA WA MWANZA LEBERATUS BARLOW YAMETAJWA
Majina ya watu watano wanaotuhumiwa kuhusika moja kwa moja na kifo cha aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Leberatus Barlow yametajwa na Polisi.
kwa mujibu wa MillardAyo.com.
Majina hayo yametajwa na Mkurugenzi wa upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Said Mwema amesema kuwa simu iliyoporwa ya mwanamama ambaye alikuwa akisindikizwa nyumbani na marehemu ndiyo imesaidia kukamilisha upelelezi huo na wahusika kukamatwa.
Waliotajwa kuhusika na hayo mauaji ni Muganyizi Michael Peter (36) ambaye ametajwa kwamba ndiye aliyemuua Barlow, Chacha Waitare Mwita (50), Magige Mwita Marwa (48), Buganzi Edward Kusuta pamoja na Bhoke Marwa Mwita (42) ambao wote wamekatwa wakiwa Dar es Saalam walipokimbilia baada ya mauaji.
.Amesema Kikosi kazi cha upelelezi kilichokuwa chini yake Manumba kilijigawa kwenye makundi matatu moja ni lile la Ukamataji, Mahojiano na jingine la intelijensia huku wakitumia njia ya sanyansi kufatilia kupitia mitandao ya simu.
Kukamatwa kwa watuhumiwa hao wa Dar na wale wa Mwanza kunafanya jumla yao kuwa 10 na bado jeshi linasaka wengine Lakini chanzo cha hao wauaji kufanya hivyo bado hakijatajwa.
Kumbuka Liberatus Barlow aliuawa Oktoba 13 mwaka huu, saa 8 usiku kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana katika eneo la Minazi mitatu huko Kitangiri alipokuwa akimsindikiza Mwalimu Dorothy Moses nyumbani kwake kutoka katika kikao cha harusi kilichofanyika Mtaa wa Rufiji.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
mmh! haya!!
ReplyDelete