1. Mwanamke anapaswa kuwa na maisha yake na sio maisha ya kuiga. Wapo wanawake ambao hupenda kuiga kile kinachofanywa na wanawake wenzake na kudhani hivyo ndivyo anavyopaswa kuwa. mwanamke mwenye tabia hiyo huwa hana mvuto kwa mwanaume kwani atakuwa ni mwanamke fake.
2. Mwanamke anapaswa kuwa mtiifu na mwenye heshima na pia mwenye busara. Mwanamke hapaswi kuwa na kiburi na kutaka kuota mapembe ndani ya mahusiano. Heshima na utiifu haimaanishi kuwa tayari kunyanyaswa, hapana. Mwanamke anapaswa ampe mpenzi wake ama mumewe heshima inayotakiwa kama kichwa cha mahusiano yenu.
3. Mwanamke anapaswa kuwa na uwezo wa kujitegemea. Hapa utata idogo, wapo wale wanaoamini kuwa mwanamke anapaswa kutegemea kila kitu toka kwa mwenza wake. lakini ukweli ni kwamba wanaume wengi wanapenda kuwa na uhusiano na mwanamke ambaye anaweza kusimama kwa miguu yake na kujitegemea.
4. Mwanamke lazima awe anajiamini. Naam, hapa haimaanishi kuwa anatakiwa kuwa kiburi na mbishi, hapana. Isipokuwa mwanamke anapaswa aonyeshe kujiamini kwa kile anachosema na anachotenda. Kujiamini kunamfanya mwanaume ajue kuwa ana mpenzi ama mke ambaye anaweza kukabiliana na mikwaruzo mbalimbali inayohitaji hoja na utetezi.
5. Mwisho, mwanamke anapaswa kuwa na mvuto. Hapa haimaanishi kuwa mrembo saaaana, hapana. Ina maana kuwa mwanamke anapaswa kuwa nadhifu kila wakati ili
kumfanya mwanaume apende kuwa nawe na avutiwe kuwa nawe wakati wote.
6. Mwanamke anapaswa kuwa na mapenzi ya kweli na huaminifu kwa mwenzie. Hapa ina maana kuwa ni lazima mwanamke amkubari mwenzie kwa kila hari, asimpende mwenzie kisa anakitufulani siku hakipo basi anamkimbia au anatoka nje ya mahusiano bila mwenzie kujua au kufanya hivyo kwani kitendo hiki huaribu mahusiano na hatimae kuleta magonjwa au mtafaruku kati yenu.
No comments:
Post a Comment