Oct 15, 2012

MWILI WA ALIEKUWA RPC MKOANI MWANZA ASCP LIBERATUS BARLOW WAAGWA LEO MKOANI HUMO

Hii ndio safari ya mwisho ya aliekuwa kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza ASCP Liberatus Barlow (53), alieuwawa juzi kwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi ameacha mjane na watoto wa nne.

Shughuli ya kuuaga mwili wake ilifanyika leo kuanzia saa Nne asubuhi hadi saa Kumi jioni katika viwanja vya Nyamagana jijini Mwanza, ikihudhuriwa na mamia ya watu kutoka jiji hilo na viunga vyake pamoja na watu kutoka mikoa ya jirani.

Vile vile Viongozi wa kitaifa waliongozwa na Waziri wa nchi ofisi ya waziri Mkuu sera na uratibu wa bunge Ndg William Lukuvi, Upande wa polisi waliongozwa na Afande DCI Robert Manumba akimwakilisha IGP Saidi Mwema.
              Maafisa wa polisi , wakiuingiza uwanjani mwili wa Kamanda Barlow.

                         Maafisa wa polisi wakiuweka sawa mwili wa Kamanda Barlow

                                    Kamanda Barlow enzi za uhai wake

                  Waziri Lukuvi akiaga Mwili wa marehemu Barlow .

          Mjane wa marehemu Kamanda Barlow ,akitoa heshima za Mwisho.

                    Sanduku liliowekwa mwili wa RPC Barlow

No comments:

Post a Comment