Maulid Ali a.k.a Mau
JICHO LAKO: Vipi kaka, kuna show yenu inatarajiwa kuanza kuonekana katika kituo cha Dar es salam Television (DTV) sijui lile Jina la kundi lenu lina maana gani?
MAULID ALI(MAU): Linaitwa MAHOKA'Z kwa lugha yetu ya kisanii lina maana ya uropokaji ama unaweza kusema faaraguzi ( uchezaji wa kutofuata script ), lakini vilevile jina hili ni la kitamaduni lenye maana ya tambiko.
JICHO LAKO: Kwanini mmeamua kutumia jina hili la kitamaduni wakati tumeona makundi mengi yakijiita majina ya kisasa?
MAULID ALI(MAU): Kisa cha sisi kujiita MAHOKA'Z ni kutokana na kuona tunamudu style zote ikiwa ni pamoja na kufuata script na kutofuata script!
Mau(kushoto) akiwa pamoja na Tin White(kulia)
JICHO LAKO: Ooh, sasa labda unaweza ukasema hilo kundi pengine linaundwa na Wasanii wa ngapi na lengo lake kubwa kwa jamii?
MAULID ALI(MAU): Kundi linaundwa na watu wa tatu ambao ni TinWhite anaesimama kama Joh, Ringo kama John na anaemaliza list ni Mimi ambae nitasimama kama Johnson na kuhusu lengo letu kubwa ni kutoa elimu na burudani kwa mashabiki wetu.
JICHO LAKO: Tunajua kuwa, kuna makundi mengi ya burudani au Comedy hapa nchini(Tanzania) sasa mmejipangaje katika ushindani huu?
MAULID ALI(MAU): Kweli tunajua kuwa kuna burudani ya vipindi vya Comedy vingi, tukianzia na channel 5 kuna Ze Comedy Show, TBC kuna Orijino Komedi, Star Tv kuna Futuhi na show nyingne kibao, but ukizifuatilia show zote hizo utagundua kuwa zinafanana maudhui! What we want tu do(Tunachotakiwa kufanya) ni kwmba show yetu itakuwa tofauti na haitokuwa kwa mfumo wa habari kama wanavyofanya wengine bali ni style ya maisha yanayotokea kila siku na itakuwa inachezwa ndani ya nyumba tu.
JICHO LAKO: Labda tutegemee kuona kitu gani humo ndani ya nyumba inayohusu show nzima, maana tumezoea kuona Mandhari(Mazingira) tofauti tofauti katika show nyingine?
MAULID ALI(MAU): Ujue nini sisi yaani Joh, John & Johnson tunaigiza ndugu wa Mama mmoja lakini kila mtu na baba yake, So tunakutana mjengoni(kwenye Nyumba) moja na kuishi pamoja tukiwa na tabia tofauti tofauti tulizozirithi kutoka kwa baba zetu na kuanza kuzionesha hapo nyumbani yani kaka ni hatari kabisa sio kitu cha kukosa!
JICHO LAKO: Ok, Mwisho labda una nini cha kuwaambia mashabiki wenu wanaowasubiria kwa hamu kubwa MAHOKA'Z?
MAULID ALI(MAU): Wategemee kitu tofauti sana na walivyozoea kuviona katika comedy show zingine za bongo na show itaanza kurushwa tarehe Novemba 2 mwaka huu saa Tatu kamaili usiku. Kauli mbiu yetu ni Cheka kwa hiari!
No comments:
Post a Comment