Oct 15, 2012

PATA ALICHOSEMA ZOLA D JUU YA UJIO WA NGOMA YAKE MPYA


JICHO LAKO: Niambie kaka, Mashabiki wako wanataka kujua kuwa baada ya kutoka Germany nini wakitegemee kwa sasa kutoka kwako?

ZOLA D: Poa sana kamanda wangu, Wategemee Ngoma yangu mpya inakuja inatwa knockout ambayo itatoka hivi karibuni chorus ikiwa imegongwa na P Funk Majani.


JICHO LAKO: Kama Majani ndio aliegonga chorus humo ndani bila shaka Ngoma itakuwa imerekodiwa katika studio ya Bongo records ambayo inamilikiwa na Majani mwenyewe sio?

ZOLA D: Yeah, Majani ndio aliefanya chorus humo ndani pamoja na kutengeneza beat na mixing kupitia studio yake ya Bongo records.


JICHO LAKO: Ok, na vipi kuhusu labda kichupa(video) cha hiyo Ngoma yako tutegemee au haitakuwa na video?

ZOLA D: Video inakuja kamanda wangu bado vipande kadhaa vya sehemu ya Majani ambavyo nategemea kushot friday wiki hii mana sehemu zangu nyingi nimeshot nchini Germany kipindi nilipokuwa huko na ningeweza kumaliza video yote ila Majani akuwepo Germany ndio maana nimeona nijekumalizia hapa nyumbani(Tanzania).

JICHO LAKO: Kuhusu kampuni inayoshot hiyo video ni ya nchini Germany au ni ya hapa Nyumbani(Tanzania)?

ZOLA D: Kampuni inayoshot Ngoma yangu ni ya kwangu mwenyewe yaani naimiliki kama Zola D na ndio itafanya kazi nzima.

JICHO LAKO: Labda hiyo Kampuni yako inaitwa jina gani na imeshafanya kazi ngapi mpaka sasa?

ZOLA D: Inaitwa Unde Video Productions, kuhusu muda bado Mpya nimeanza kushot video mpya ya Mb Dog itatoka soon on air na kuna kama kazi tano za wasanii wakubwa wa kenya najipanga kushot.

No comments:

Post a Comment