Waigizaji filamu nchini Tanzania Wema Sepetu na Aunt Ezekiel, jana wamewaomba radhi Watanzania wote kutokana na picha za nusu utupu walizopigwa hivi karibuni katika Tamasha la Fiesta lilipofanyika mkoani Dodoma. Warembo hao waliyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar.
Kwa upande wa Msanii Aunty Ezekiel amesema kuwa wao wameumia sana kwa kuonekana kwa picha zile kwa sababu wao kama wanawake katika jamii, wana wazazi, Ndugu, jamaa, marafiki pamoja na mashabiki mbalimbali wa kazi zao ambao wanawaheshimu kuliko baadhi ya watu wanavyofikiria. Ameongeza kuwa alikuwa amelewa hivyo basi ni vyema Watanzania wakawasamehe kwa kitendo hicho hakitoweza kujirudia tena kwani kimewatia aibu sana.
Wema akiwaomba radhi watanzania juu ya kitendo cha kupigwa picha zilizoonesha nguo zao za ndani wakiwa jukwaani mkoani Dodoma katika tamasha la Fiesta.
Wema(kulia) na Aunt Ezekiel(kushoto) wakiwa katika jukwaa la Fiesta ambapo ndio siku iliopigwa picha ya Kuonesha nguo ya ndani ya Msanii mahiri wa filamu hapa nchini Aunt Ezekiel.
No comments:
Post a Comment